#8.
Eleza Hadithi

PICHA HAZIFUTIKI: KUWA MWANGALIFU KWA PICHA UNAZOTUMIA

Mara tu picha zimechapishwa, haziwezi kurejeshwa tena. Ufikiaji wa wavuti kwa watu wote unaweza kuwaweka watu katika hatari za aina nyingi.

Unaporipoti kuhusu ukatili  wa kijinsia katika migogoro ni muhimu kuchagua vizuri video au picha unazozitumia. Hasa sasa katika enzi ya dijitali, picha zina kaa muda mrefu kuliko visa unavyoripoti. Ni muhimu kwamba wahasiriwa waelewe kikamilifu jinsi watakavyowasilishwa kwa picha auvideo na nini matokeo yake. Unapaswa kuzingatia:

  • Je, kuna haja kubwa ya kuwatambulisha wahasiriwa au ni salama kwanza kuripoti bila wao kujulikana?
  • Je, wametoa idhini yao halisi kupigwa picha au kuchukuliwa video? Je, wanaelewa ufikiaji wa mitandao ya kijamii ambayo inaweza kuonekana katika jamii zao?
  • Je! Kuna kitu chochote kwenye picha ambacho kinaweza kufunua utambulisho wao bila kukusudia?
  • Ninawezaje kuwashirikisha katika kutengeneza picha ili waridhike na nakala za mwisho?
  • Na jambo la kimsingi la maadili: je, ningefurahi mimi au mtu wa familia yangu kupigwa picha au video hivi?

Acha niwe wazi, picha za ubakaji katika migogoro na  wahasiriwa wa ubakaji zinahitajika kusambazwa kwa wingi. La muhimu ni kupigwa kwa njia ambazo zinalinda wahasiriwa, kwamba picha zinaheshimu muktadha, picha  haziendelezi kasumba potofu, na hazijawasilishwa na vyombo vya habari kama suluhisho mwafaka kwa wahasiriwa. [a

Picha ni sehemu muhimu ya kuripoti migogoro, ikiwemo ukatili wa kijinsia katika migogoro, na inaweza kuwa njia nzuri sana ya kuleta uhusiano kwa wasomaji. Lakini pia kuna uwezekano mkubwa wa kudhuru wahasiriwa mbali na hatari ya kuwahoji. 

Kuna historia ndefu ya picha za kibaguzi ambazo ni za kutoka enzi za ukoloni na utumwa na kwa hivyo kuelewa kuhusu matumizi ya picha ni muhimu.

Kwa kuongezea, Picha zinasambazwa kwa urahisi katika enzi ya dijitali, kwenye vifaa tofauti na kwenye majukwaa yote. Hii inamaanisha kwamba wahasiriwa wanaweza kusumbuliwa hata kama wanaishi vijijini na kwa miaka ijayo. Kwa mfano, katika vita vya Balkan vya miaka ya tisini, kulikuwa na visa ambavyo wanawake waliolewa bila kuwaambia waume zao kwamba walikuwa wamebakwa… Miongo kadhaa baadaye, wachache walikuwa na wazo kwamba nyenzo za kumbukumbu zinaweza bado kupatikana mtandaoni.

Enzi ya dijitali pia inatoa nafasi ya habari zinazoambatana na picha na hivyo kuleta shinikizo kwa wahariri na wapiga picha kutumia picha za kusisimua zaidi na za kuvutia. Hii inaweza kusababisha picha zinazochochea mwili wa mhasiriwa, au kuzitambulisha bila haja. 

Linapokuja suala la wahasiriwa wa ukatili wa kijinsia katika migogoro, vielelezo vya picha ni kawaida – kuonyesha mhasiriwa akiwa ametengwa na kufanyiwa ukatili, ametolewa kutoka kwa mazingira yao, au kuzingatia sana mwili wake. 

Kama ilivyojadiliwa hapo awali katika kifungu cha #3 kuhusu idhini, kuwashirikisha waliohojiwa katika maamuzi kuusu jinsi wataonyeshwa,h ni mazoezi mazuri. Wanahabari wakiripoti kuhusu ubakaji wa wanawake wa Yazidi  na ISIS waldhani walihakikisha kutojulikana kwa wanawake hao kwa kuwapiga picha wakiwa wamefunikwa nyuso, lakini kwa kweli, walikuwa  wakitambulika kwa urahisi ndani ya jamii zao kwa macho yao na mitandio tofauti.

Kufanya uchaguzi mzuri zaidi na maadi ya kuona

Ingawa wapiga picha wa vyombo vya habari mara nyingi wanafanya kazi na shinikizo kutoka kwa ofisini ili kupata picha yenye athari zaidi, inawezekana kuchukua picha za wahasiriwa wa ukatili wa kijinsia  ambazo zinaweza kuepusha madhara kwa mhojiwa hata kama wakati ni mchache. Hapa kuna maswali ya kujiuliza juu ya picha unazochukua:

  • Je, unaweza kuanza na dhana kwamba picha zozote za wahasiriwa hazitajulikana, na kwamba watatambuliwa tu ikiwa kuna sababu kubwa ya kufanya hivyo? Jadili jambo hili kwa undani na mhariri wako kabla ya kufika unakoenda.
  • Kuna njia nyingi imara na za ubunifu za kuchukua picha ambazo haziwatambulishi wahasiriwa. Ni bora kufikiria haya mapema kabla ya wakati. Labda uanaweza kuweka albamu ya dijitali kama wengine wanavyofanya.
  • Kwa kuwa ripoti hiyo inahusu ubakaji, unapaswa kufahamu jinsi unavyoonyesha mwili wa mhasiriwa. Je, ni sehemu gani ya mwili unayotaka ionekane na ni jinsi gani unaweza kuzuia kuonekana kwa mhasiriwa kama kitu cha ngono?
  • Jaribu kutafuta njia inayoepuka picha ambazo  zinazoonyesha kuwa mhasiriwa ni mpweke au ameangamizwa. Wakati mwingine fikra ya kutengwa sana inaweza kuwa ndio ukweli wa mambo, lakini kawaida watu huwa na muktadha mpana wa msaada – na ni vizuri zaidi kuonyesha hilo.

Ikiwa unatumia mbinu za dijiti kuficha utambulisho, saizi asili zinahitaji kuondolewa kutoka kwenye picha, sio tu kuwa ukungu; na kwa kweli, hakikisha kuwa hakuna data meta katika faili ambayo inabainisha eneo.

Ni muhimu pia kufikiria ni nani anaweza kuwa karibu wakati picha zinachukuliwa na kwanini? Hapa kuna vidokezo vya kuzingatia:

  • Je, anayehojiwa angependa kuwa na mtu pamoja naye au kuna watu ambao hawapaswi kutazama? Kwa watengenezaji wa filamu, jaribu kupunguza wasaidizi wa kazi.
  • Baada ya picha hizo kuchukuliwa, ni vizuri kuwaonyesha wahasiriwa ili kuwaruhusu waeleze ikiwa wanaridhia na vile picha zimepigwa.
  • Hakikisha wahasiriwa wanaelewa kuwa picha zao zinaweza kudumu kwa muda mrefu sana na kwamba zinaweza kusambazwa kwenye majukwaa mengi yakiwemo katika jamii yao.

Je, kuna njia za kutokuharakisha kazi hio? Je, unaweza kujadili jinsi upigaji picha utafanya kazina kuelezea itachukua muda gani? Kumbuka kwamba watoto hawawezi kamwe kutoa idhini ya kuonyesha utambulishi wao hata kama mtu mzima ametoa idhini.

Uanahabari wa picha na Wahariri

Ninaweza kuelewa jinsi mpiga picha anavyoweza kukosa kufahamu haya, lakini sitarajii hilo kutoka kwa mhariri. Ninahisi kuwa kwa wahariri wana uwajibikaji zaidi wa  kuelewa kuhusu picha kulingana na muktadha wa kihistoria. 

– Nina Berman [a

Wapiga picha huwa na uhusiano na wahasiriwa na hufanya maamuzi kuhusu matumizi ya picha. Lakini wahariri hubeba jukumu la mwisho kwa picha ambazo zimeagizwa na kuchaguliwa kutoka kwa picha nyingi kabla ya kufikia umma. Kinachoweza kufaa kwa ukarasa wa ndani – ambapo ina maana na muktadha – inaweza kuwa na athari tofauti kabisa ikiwa inasimama peke yake kwenye kifuniko au chapisho la Instagram.

Kwa kutumia utaalam na wakati wa kufikiria kimkakati mbali na shinikizo za uwanjami, wahariri wanapaswa kuzingatia namna ya picha itaonyeshwa kwa makusudi au bila kukusudia. Kwa mfano, kuna historia ndefu ya picha za watumwa ambazo waandishi wa habari wanaofanya kazi katika nchi zinazoendelea wanapaswa kuziepuka. 

Wahariri wa picha wanaweza pia kuwa na nguvu ya kufanya maamuzi juu ya nini kittendeka baadaye kwa picha – leseni yake na upatikanaji – na pia njia ambayo inatumika kwenye mitandao ya kijamii. 

Wahariri,  Wanaweza kuwa wamefanya kazi na wafanyikazi wenzao wa muda mrefu, au kuwaagiza wapiga picha huria ambao hawajawahi kukutana nao. Kupata wakati wa mazungumzo mafupi ya dakika 10 juu ya mipaka, idhini halisi, na kutokujulikana kunaweza kuleta mabadiliko makubwa.

Hapa kuna mambo ya kuzingatia:

  • Je! umekuwa na mazungumzo yakutosha na wapiga picha kuhusu idhini?

  • Je! kuna haja ya wahasiriwa kutambuliwa? Je, aina gani ya picha utatumia wakati wa kuhifadhi kutokujulikana?

  • Maelezo mafupi ya picha ni sehemu ya ripoti na kama picha, hayapaswi kumdunisha au kumnyanyapaa mtu huyo.
  • Je! unaweza kutoa muda wa picha za wahasiriwa wa ukatili wa kijinsia katika migogoro? Je, unaweza kuzifanya zitumike mara moja tubila kuuzwa kwa wakala?
  • Je, picha hizo zitatumiwaje kwenye mitandao ya kijamii? Je, unahitaji kuonyesha uso au mwili wa mhasiriwa kwenye Instagram, kwa mfano, au kuna njia nyingine ya kuhamasisha kisa, yenye haimwachi mtu aliye hasiriwa kubeba uzito wake wote?  

Maelezo ya chini: