#7.
Eleza Hadithi

KUMBUKA: UNYANYASAJI WA KIJINSIA SIO MWELEKEO PEKEE WA HADITHI KWENYE TUKIO

Kuzingatia sana ukatili wa matukio peke yake inaweza kuleta athari mbaya kwa wale unawahoji na uandishi wa habari kwa jumla. Kuwa mwangalifu kwa muktadha kamili.

Baada ya kukabiliwa na hofu kubwa kama vile ubakaji wa watu wengi katika vita au utumikishwaji wa biashara ya ngono, mwanahabari anaweza kuhisi kama ni kawaida kuweka mwelekeo wote juu ya vurugu za kijinsia na madhara ambayo husababisha. Lakini kushindwa kuangazia muktadha mpana kunaweza kufanya ripoti yako kuwa finyo hivyo kuwapoteza watazamaji na pia kuwatenga wahasiriwa. Na kwa hivyo hakikisha kupanua ripoti yako kwa njia zifuatazo:

  • Toa maelezo kamili kuhusu maisha ya wahasiriwa. Kuwa mwangalifu usitabiri uharibifu au kudhalilisha wahasiriwa kwa mambo mabaya yaliyowapata. Jambo hili linaweza kufanya vigumu wao kupona.
  • Fikiria kuwa kuna uhalifu mwingine zaidi ya ubakaji. Wahasiriwa wanaweza kupoteza wapendwa wao, nyumba zao, na kuhamishwa kwa nguvu. Vitu hivi ni muhimu kwa watu pia.
  • Epuka kuzingatia kupita kiasi habari ambazo zinaweza kufanya kisa kuwa cha kingono/au cha kusisimua. Hili linaweza kupunguza huruma ya umma kwa wahasiriwa.
  • Saidia hadhira yako kuona njia za suluhisho zinazowezekana kwa kutendae haki kwa muktadha kamili wa kisiasa na kijamii.

Mara nyingi tunapuuza jinsi kazi yetu inaweza kusaidia wahasiriwa na hata kuwa na athari juu ya jinsi wanavyopona. 

Ukatili wa kijinsia unahusishwa na viwango vya juu vya kisaikolojia na vile vile maumivu ya kimwili. Matokeo ya jeraha la kijinsia kawaida huleta hisia kali za kujitenga, ambayo watu huhisi wamejitenga na wao wenyewe – mtu aliyvokuwa kabla ya yote kutokea – na pia kujitenga na wengine. Uwezekano wa watu waliopatwa na ukatili wa kijinsia kukata uhusiano na jamii pana inaweza kuacha wahasiriwa wakiwa wametengwa na hivyo kupunguza nafasi za msaada. 

Kwa upande mwingine, ili kupona inaonekana kinuyme cha hiki kinahitajika. Inatokea kupitia kuunganishwa tena, wakati watu wanaamini kuwa inawezekana tena kwa wengine kuwajali na kuwaheshimu. 

Kama wanahabari, sio jukumu letu kuponya watu – na haitakuwa busara na itakuwa kama dharau kudhani kwamba kazi yetu itawasaidia wahasiriwa kwa njia ya moja kwa moja. Hata hivyo, tunapaswa kuzingatia ili tusiongeze hizo nguvu za kuvunja uhusiano bila kukusudia. Jina Moore, mwandishi wa habari wa Amerika ambaye anafanya kazi Afrika Mashariki, anaandika hivi: 

Tunapaswa kuhakikisha kuwa hakuna chochote katika ripoti tutakayochapisha – kwa siku, miezi, na mwaka – ambayo inashangaza, inatia aibu, fedheha au inawahatarisha … Lengo la kurudia maelezo ya kisa cha cha mhasiriwa ni kuhakikisha kwamba anaelewa kile watu wengine watajua juu yake. [a]

Ujumbe ambao tunatuma kwa hadhira iayolengwa pia ina umuhimu mkubwa. Kila mahali majadiliano kuhusu tukio la kiwewe la kijinsia yanaandamana na hadithi za uwongo, unyanyapaa na kasumba zisizo na usaidizi. Tunaweza kuziimarisha au kuonyesha ukweli kuhusu kasumba hizi- wanahabari na watengenezaji wa sinema sio watazamaji tu bila kuwa na hisia zao. 

Hii ndio sababu kuwa ufahamu kamili juu ya muktadha wa kisiasa, kiuchumi, na kitamaduni wa mzozo ni muhimu.

Hatari ya kuangazia upande mmoja tu wa kisa

Tukio la ukatili wa kingono unaeza kufanyika katika aina tofauti lakini mara nyingi kitu kinachoonekana zaidi ni ukatili wake. Kama mtengenezaji wa filamu au mwanahabari, unaweza kupata hamu kali ya kusisimua hadhara inayolengwa kwa kutumia mabaya ya yale uliyosikia kwa matumaini ya kuwaamsha. Hili ni jambo linaloeleweka kabisa. 

Lakini hatari iliyopo ni kwamba hii inaweza kuleta madhara. Kuzingatia sana kuhusu tukio la kutisha na undani wa ukatili wa kijinsia, kunaweza kulazimisha hadhira inayolengwa kuacha kutilia maanani na kujitenga kwa njia ambazo zinaweza hata kupunguza huruma kwa watu walioathiriwa na ukatili wa kijinsia katika migororo. Kama hakuna habari ya kutosha, hadhira inayolengwa haitaelewa hali ya uhalifu huu na ni nini kiko hatarini. 

Kwa Stephanie Kariuki, ambaye alikuwa akifanya kazi na Podcast for Vice ambayo ilichunguza unyanyasaji wa kijinsia huko Misri na jukumu la serikali katika kuendelea kwake, maamuzi haya yanahitaji kusawazisha kwa uangalifu mambo haya:

Kulikuwa na mambo mengi kuhusu  ufafanuzi wa ziada unaotakinana? Kwa nini tunatoa maelezo, na ni muhimu kweli? …. Kwa mfano, walichunguza uke wa mwanamke mara nne. Hilo ni jambo la kindani sana kutaja – na mara nne ni nambari imeambatanishwa nayo. Na sababu ya sisi kwenda kwa undani kama tunavyofanya ni kwa sababu uchunguzi huu ambao anapitia ni ishara ya kile serikali ilikuwa ikifanyia wanawake kwa miongo kadhaa. [b]

Hakika, kuandika kwa ufanisi juu ya matukio ya kiwewe inahitaji kujua jinsi ya kusawazisha masuala tofauti ambayo yanapingana. Kwa mfano:

  • Je, ni kiasi gani mtaongea kuhusu madhara, kukosa msaada, na upotezaji wa udhibiti ambao ukatili wa kijinsia unaleta kwa maisha ya wahasiriwa? Au ni kiasi gani mtaongea kuhusu upinzani na kupona- ilihitaji nini, na inahitaji nini kuishi?

Hata kama inaonekana mbaya, wahasiriwa wana mambo mazuri yanayoendelea katika maisha yao. Kuonyesha tu matukio ya kutisha na kutokuwa na nguvu  sio jambo sahihi wala la kusaidia.

  • Je, ni kiasi gani itakuwa kuhusu matukio aliyopitia mhasiriwa na ni kiasi gani juu ya muktadha mpana – haswa hali ya kisiasa na kijamii?

Kukosa kuzingatia kikamilifu muktadha mpana kutafanya ripoti  kuwa kisa cha kuleta hisia ya kibinadamu ya aina ya kushangaza na ya kusumbua – ripoti ambayo haina lengo maalum na ambayo haiwapi hadhira inayolengwa uelewa mzuri wa kile kinachotokea na suluhisho. Ukatili wa kijinsia haufanyiki bila matukio mengine – mada kamaubakaji vitani haieleweki bila kutaja matukio yanayochochea mzozo. 

Kwa upande mwingine, kutowapa watu uzingativu kamili kwa hali zao za kibinafsi pia inaweza kuonyesha kukosa heshima, kwani inaweza kutoa taswira kuwa mtu alijumuishwa tu ili kuwa kama takwimu fulani.

Kujadili mivutano inayokinzana

Kila kisa kitahitaji mizani tofauti. Kuelewa hili jambo mara nyingi ni vigumu kwa sababu ya  athari ya vurugu ambayo inaweza kutupelekea kuona kila kitu hakina maana. Habari za kutisha za kiwewe huwa zinakuza fikra finyu. Ni rahisi sana kukwama kwenye maelezo au pande kidogo. 

Hapa kuna orodha fupi ya kuangalia wakati unapoandika au unahariri: Je, hii inaingia ndani sana katika maelezo ya picha ya kimwili au ya kibinafsi?

  • Je, kuna maelezo kuhusu mwili wa mtu, muonekano, mavazi, nk, ambayo yana hatari ya kuifanya maelezo ya kingono  (na hata kuidhinisha motisha ya unyanyasaji)?
  • Je, kisa hiki kinaweza kutabiri uharibifu wa baadaye wa mtu au jamii? Hata kama mambo yanaonekana mabaya, sio sahihi na kuhukumu kuwa haiwezekani kupona. (Ikiwa unapata shida kuona chochote kizuri, jiulize kuna nini kizuri kwa mtu huyu zaidi ya unyanyasaji? Wanapata wapi ujasiri na msaada)?
  • Kwa upande mwingine, je, ninachukua mkondo wa kinyume na kutoa matumaini ya uwongo kwa nia ya kupunguza makali ya hali mbaya? Mbali na shida iliyo wazi kuhusu usahihi, uandishi wa habari unaotilia chumvi uwezeshaji unaweza kuwatenga wale ambao hawatambui hali zao.
  • Ikiwa makala yangu yanajumuisha sauti za wahusika na wahasiriwa, je, kuna chochote katika kueleza ripoti yangu ambacho kinazingatia sana kuhusu wanyanyasaji au inaongeza nguvu zao? (Kupata hili sahihi ni kazi ngumu. Kutenganisha sauti hizi kwa ripoti tofauti inaweza kuwa rahisi zaidi).
  • Je, masimulizi yangu ynazingatia zaidi ubakaji na kupuuza shida zingine ambazo watu hupitia wakati wa vita na migogoro? Huenda kule wale wameona jamaa zao wakiuawa na kupoteza nyumba zao na kazi. Wanaweza kuwa ni wakimbizi wanaojitahidi kujenga maisha mapya. Vitu vyote hivi ni muhimu kwa watu, na wahasiriwa wanaweza kukosa kuelewa kwa nini mwanahabari na anachukua muelekeo wa upande mmoja.

Namna Ya Kueleza Ripoti: Maelezo Kwa Wahariri 

Njia ambayo habari inatolewa – kichwa cha habari, maelezo mafupi ya picha, picha zinazotumiwa kutangaza filamu, muhtasari, njia inayowasilishwa kwenye mitandao ya kijamii – inaweza kuwa na athari kubwa kwa jinsi habari inapokelewa na athari yake kwa watu ambao wamehusishwa na habari hio.

Hatari moja iliyo wazi ni kuifanya ripoti ionekane kama ya ngono – kuifanya iwe ya kusisimua kwa njia ambayo inaitoa kwenye muktadha halisi. Katika ukatili wa kijinsia, ngono inaweza kutokea – lakini matukio haya sio kwa njia yoyote kama ngono ya kawaida. 

Maneno kama ‘watumwa wa ngono’ ni ya kuogofya na ina hatari ya kugeuza unyanyasaji kuwa burudani. Maneno kama “bibi harusi watoto” ni vizuri ikielezewa  kama “kutekwa nyara na unyanyasaji wa kijinsia wa mtoto.” Mtu ambaye amelazimishwa kufanya ukahaba sio mpenzi. 

Hapa, Jineth Bedoya, ambaye ameandika sana kususu ukatili wa kijinsia huko Amerika Kusini. Anaelezea jinsi mifumo ya ukatili wa kijinsia unaofanywa na wanamgambo imefichwa nyuma ya lugha isiyofaa na ya zamani kama: 

Tumefanya kampeni kali kwenye vyombo vya habari ili waache kutumia neno ‘uhalifu wa mapenzi’ wakati wanahabari wanataja ubakaji au mauaji ya wanawake.

Jamii bado inatizama ubakaji kuwa unahusishwa na uchochezi wa kijinsia ambao mwanamke analenga kwa makusudi kwa mwathiriwa wake. Ndio maana kutumia neno “mapenzi.”

Lakini kwa kweli, uchochezi hapa ni lile wazo katika aina hii ya uanahabari kwamba uhalifu kama huo unafanywa kwa jina la mapenzi.

Katika kesi nyingi nimesikia wanaume wanaobaka wakijitetea kwa hoja hii. Wanasema kwamba “waliwanyanyasa kijinsia,” au kuwaua kwa sababu waliwapenda.

Jihadhirini pia kwamba upangaji wa ubakaji kama matokeo ya kuepukiya vita ni hadithi. Mbali nakuwa uhalifu wa kivita unaostahili adhabu, utafiti unaonyesha kwamba haujaenea katika mizozo yote, hata pale wapiganaji wa kawaida.[c]

Popote unapoweza, jumuisha rasilimali za mashirika ya msaada na habari ambayo inaweza kusaidia mtu yeyote ambaye ni mhasiriwa wa ukatili wa kijinsia kusoma au kutazama kipande hicho.

Rasilimali Za Ziada:

Katika Mtego wa Ponografia, Jina Moore alizungumzia changamoto za kupata lugha sawa. Zana kutoka kwa Kikosi cha Kazi cha Chicago juu ya Ukatili Dhidi ya Wasichana na Wanawake Vijana inajadili kuripoti kwa unyanyasaji wa kijinsia kwa jumla na ina sehemu inayoonyesha juu ya uchaguzi wa lugha.

Makala haya kutoka kwa Kituo cha Kitaifa cha Rasilimali za Ukatili wa Kijinsia na pia inashughulikia aina zote za unyanyasaji wa kijinsia huko Merikani na hainauhusiano wowote ule na Vurugu za Kijinsia zinazohusiana na migogoro, (CRSV). Lakini, inaonyesha nguvu ya kuchukua mbinu inayoongozwa na muktadha wa kitakwimu.

Kwenye wavuti ya Kituo cha Dart, Nina Berman aangazia umuhimu wa muktadha na juu ya kufanya upelelezi unaofaa wa kuona — haya yote yamefafanuliwa zaidi katika sehemu inayofuata.

Maelezo ya chini:

  • a

    Katika makala ya Jina Moore: Mtego wa Ponografia.

  • b

    Kariuki alishiriki katika utafiti wetu kuhusu suala hili.

  • c

    Carlos Koos (2017) Ukatili wa kijinsia katika mizozo: maendeleo ya utafiti na mapungufu iliyobaki, Ubora wa Dunia ya Tatu, yapatikana hapa.