Kwa nini hii?

Miongozo hii imeibuka kutokana na mazungumzo kadhaa kati ya wanahabari wenye uzoefu na watengenezaji wa filamu ambao wamefanya kazi mara kwa mara kwa muda mrefu kwenye hadithi zinazohusu unyanyasaji wa kijinsia na mateso katika nchi zilizo athirika na migogoro. 

Bila shaka kila mtu anyefanya kazi hii ana nia nzuri. Lakini wakati fulani sisisote  tunaweza kujiuliza ikiwa kuna uwezekano kwamba tunaweza kuwa tuna wadhuru watu ambao hadithi zao tunajaribu kuripoti. 

Wanahabari, ambao mara nyingi huwa wa kwanza kuhoji wahasiriwa wa ukatili wa kijinsia katika maeneo ya migogoro lakini mara nyingi hawapati mafunzo yoyote ya msaada ambao wanahitaji kufanya kazi hii kwa usalama na kwa ufanisi.

Ndio maana tukatayarisha muongozo huu. Miongozo hii inaangazia masuala nane muhimu ya ujuzi ambayo tuna imani kwamba  kila mwanahabari  au mtengenezaji wa filamu anayefanya kazi kwenye maswala yanayohusiana na ukatili wa kingono anahitaji kufahamu. Mapendekezo haya manane yameundwa kusomwa kwa kina na katika muundo unaoruhusu kutumiwa kama msingi wa mrekebisho -na kusambazwa kwa wafanyakazi wenza. Mapendekezo hayo yamekusudiwa kuwa ya manufaa na kujibu hali halisi juu ya ardhi. 

Ijapokuwa mapendekezo haya yaliandikwa na wanahabari kwa ajili ya wanahabari, yametokana na mazungumzo pana. Wakati wa kuunda nyenzo hizi, tuliwasiliana na manusura wa mizozo unyanyasaji wa kijinsia (ambao wengine ni wanaharakati lakini wote ni wataalam), daktari wa maswala kiwewe, wafanyikazi wa jamii, wanasheria, wapiga picha, watengenezaji wa filamu, wanahabari na wahariri. 

Hili ni swala ngumu.  Wala miongozo hii haitaangazia kila hali anayokabiliwa na mwanahabari.

Hata hivyo, tumejaribu sana kusawazisha mambo haya mawili. La kwanza ni kwamba kama vitendo hivi vya ukatili havitaripotiwa, itakuwa vigumu kuvikomesha. La pili ni kwamba linapokuja suala la ukatili kingono, kila mhasiriwa ana masimulizi yake – sio sisi tunamiliki habari hizo.

Kipi kinafuata?

Tuliunda miongozo hii ili kutoa nafasi ya majadiliano na pia ili kuhamasiha watu. Lengo la miongozo hii ni kusambazwa Na kwa hivyo tafadhali sambaza kwa mtu yeyote ambaye anaweza kufaidika 

Ikiwa unataka kujua zaidi kuhusu kazi ya Kituo cha Dart, tafadhali jiandikishe hapa. Tunakaribisha maoni yako na tunatarajia mazungumzo huko mbele. 

.

Shukrani na utambuzi

Soma ili kujua jinsi rasilimali hii iliandikwa.

Ona zaidi Angalia kidogo

Miongozo hii imetayarishwa na Dart Center Europe ambao ni mtandao na rasilimali kwa wanahabari na watengenezaji wa filamu ambao hushughulikia masuala ya kiwewe na vurugu. Kwanza tunatoa shukrani  kwa kila mtu ambaye amechangia mazungumzo ya Kituo hiki kwa miaka hii yote. Timu kuu ya kuandaa na kuandika: Gavin Rees, Samira Shackle, Stephen Jukes, Juliana Ruhfus, Leslie Thomas na Christina Mwanakondoo.

Tunatoa shukrani pia kwa kila mtu ambaye alishiriki katika mashauriano yetu ya moja kwa moja. <!– Majina yao yameorodheshwa katika ripoti yetu. [Jump to page url] –>

Mradi huu uliwezeshwa kupitia ufadhili wa Ofisi ya Jumuiya ya Madola ya Kigeni na Ofisi ya Maendeleo kitengo cha  Mpango Kuzuia wa Ukatili wa Kijinsia.

KILICHOSEMWA NA WENGINE

Soma kile wengine wamesema kuhusu miongozo hii.

Ona zaidi Angalia kidogo

“Quis vel eros donec ac odio. Quis enim lobortis scelerisque fermentum dui. Tellus orci ac auctor augue mauris augue. Lacus luctus accumsan tortor posuere ac ut. Curabitur vitae nunc sed velit. Fringilla ut morbi tincidunt augue interdum. Nibh cras pulvinar mattis nunc sed. Vulputate odio ut enim blandit volutpat. Sed augue lacus viverra vitae congue eu. Scelerisque eleifend donec pretium vulputate sapien nec sagittis aliquam. Quam quisque id diam vel.”

Dart Centre Europe 
Nambari ya usajili wa hisani nchini Uiengereza na Wales: 1172731
Tafadhali wasiliana nasi. Tunakaribisha maoni.