#1.
Maswali matatu ya msingi.

JE! NIMEJIANDAA VYA KUTOSHA KWA JAMBO HILI?

Kuzungumza na vyombo vya habari juu ya ukatili wa kijinsia kwenye maeneo ya migogoro ni hatari kubwa kwa aliyenusurika. Miongozo hii itakupa fikra nzuri kuhusu kile kilicho hatarini.

Kuripoti kuhusu unyanyasaji wa kijinsia ni mojawapo ya kazi yenye changamoto kubwa  kwa wanahabari na inahitaji uangalifu wa hali ya juu. Kabla ya kuanza, hakikisha unafanya utafiti kuhusu mambo yafuatayo:

  • Ukatili wa unyanyasaji wa kijinsia ni nini na vipi ubakaji unaathiri watu binafsi na jamii zao.
  • Jinsi ya kuhoji wahasiriwa wa kiwewe kwa njia ya kuzingatia hisia zao.
  • Nguvu za kisiasa na picha ya ujumla ya usalama katika eneo , mienendo ya kijinsia,  pamoja na mitazamo ya kitamaduni kuhusu ukatili wa unyanyasaji wa kijinsia.
  • Changuo lakuona ambalo unaweza kuhitaji kufanya. Je, utapiga picha au kuchukua filamu za watu. Jinsi na wapi? Je, watatambulishwa au la?
  • Unamiliki Kiwango chako mwenyewe cha utayari wa kisaikolojia na kwanini hiyo ni muhimu.

Tumeita mwongozo huu Kuripoti juu ya Ukatili wa Kijinsia kwenye migogoro lakini katika maandishi haya tunatumia kifupi kwa lugha ya kiingereza CRSV (Ukatili wa Kijinsia kwenye migogoro). 

Ukatili wa Kijinsia kwenye migogoro inamaanisha vitendo vya ukatili wa kingono kama vile ubakaji, ukahaba wa kulazimishwa, ndoa ya kulazimishwa, uhasishwaji wa lazima na uhalifu mwingine kama huo ambao unaweza kuhusishwa na vita. Kwa kawaida, uhalifu huu hufanywa kwa malengo ya kijeshi au ya kisiasa yaliyotafakariwa – na kwa hivyo huingia chini ya vikundi vya kisheria vya mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita; lakini matukio yanaweza pia kuwa nyemelezi zaidi. Ukatili wa kingono kwenye migogoro una maana pana kuliko neno “ubakaji katika vita”. Neno hili pia linatumika kwa hali zisizo thabiti ambazo waasi, wanamgambo au vikosi vya serikali hutumia ukatili wa kijinsia kama chombo cha kugandamiza wenyeji wa eneo na kuwachochea wapiganaji. Hili hutokea kwa wanaume, wanawake na watoto. 

Uhalifu huu una athari mbaya kwa walionusurika na jamii zao hasa kwa sababu ukatili huu unaweza kutenganisha uhusiano wa kijamii na kufanya watu kutengwa na familia, marafiki na majirani ambao wangeweza kutoa msaada na kusaidia kupona. Pia ina athari za kizazi kwa watoto waliozaliwa kutokana na ubakaji na inaweza kusababisha unyanyapaa unaoendelea na vurugu zaidi kwa njia ya kile kinatambulika kama mauaji ya heshima ya kibinafsi.

Jukumu letu kama wanahabari na watengenezaji wa filamu sio ujasiri

Mara nyingi wanahabari huwa wa kwanza kuhoji manusura na katika kuangazia mambo ambayo watu wanapaswa kujulishwa, wanahabari wanajipata katika hatari kubwa kibinafsi. Ingawa hakuna mwandishi wa habari anayefanya kazi hizi anayetaka kusababisha madhara kwa wale wanaowahoji bila makusudi, lakini kuna uwezekano wa madhara kutokea. Hata kwa nia njema, makosa katika kuhoji na kuripoti yanaweza kuwafanya manusura kuona kama wametengwa na kutumiwa vibaya na pia inapelekea wahojiwa na familia zao kupatwa na aibu na hata wakati mwingine kupelekea kutendewa vurugu. 

Mnamo 2018, ripoti ilichapishwa ambayo ilifanya kitu kisicho cha kwawaida kwa kuuliza wahasiriwa wa ukatili wa kijinsia katika eneo la vita tajriba yao baada ya kuhojiwa na wanahabari. Majibu yao yalikuwa ya kusisimua. Asilimia themanini na tano walikumbana na mbinu za kuripoti ambayo zilikiuka miongozo miwili bora ya wanahabari amabyo iliyochapishwa na  Kituo cha Dart na yingine iliyofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa linalofanya kazi kwa ulinzi wa wahasiriwa.[aMasuala yaliyoainishwa katika ripoti hiyo ni pamoja na:

Ukiukaji dhahiri kwa njia ya ahadi za pesa au msaada, kufichua utambulisho bila idhini, au kushinikizwa kutoa maelezo ya kitendo cha ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia, kuuliza wanawake maswali ya kibinafsi na ya kindani kuhusu mashambulio hayo. Hali kadhalika, wanahabari walionyesha ishara walikuwa katika nafasi ya kusaidia jamii ya Yazidi kwa kuchapisha habari za wanawake wahasiriwa.[b]

Ni kawaida kwa wanahabari kupata mafunzo kuhusu mazingira ya uhasama ili kuwandaa kujiweka salama katika hali za hatari. Kwa upande mwingine, wanahabari wengi bado hawapati mafunzo stahiki na mwongozo katika kufanya kazi na wahasiriwa wa kiwewe.

Je, ni yapi maandalizi mema?

Katika safari yoyote ya kuripoti, haswa katika eneo lenye hatari kubwa, wakati ni wa thamani sana na inafaa kufikiria juu ya mambo haya mapema wakati una nafasi ya kufanya hivyo. Maandalizi ni ya aina mbili na yote ni muhimu:

  1. Aina ya maandalizi yanayohitajika kabla ya kuanza safari. Kufanya utafiti wa ndani, tathmini ya hatari, na kadhalika. 
  2. Kujitolea kwa muda mrefu ili kuimarisha ujuzi wa kazi. Hii hutokana na mafunzo na kujitolea ili kuelewa masuala na uwazi wa kubadilishana mawazo na wafanyikazi wenzako wengine.

Maandalizi yanayohusiana na kazi maalumu

Huenda una uzoefu wa kufanya tathmini ya hatari kwa usalama wako na wa timu yako kabla ya kusafiri. (Ikiwa sivyo, tafadhali angalia kisanduku hapa chini). Wakati huo huo, wakati unaripoti kuhusu ukatili wa kijinsia, unahitaji pia kuzingatia jinsi namna ya kuripoti inaweza kuathiri usalama wa kimwili na kisaikolojia wa wale unaowahoji. 

Maswali ya kujiuliza:

  • Je, umechunguza mienendo ya nguvu za kisiasa na hali ya usalama kwenye eneo  itakayokufanya uweze kufanya maamuzi mazuri sio tu juu ya usalama wako mwenyewe, bali pia usalama wa wale unaowahoji? [Tazama #2]
  • Nani atawezesha mahojiano yako na manasura? Je, itakuwa mpatanishi, asasi isiyokuwa ya serikali au washawishi wa kisiasa?
  • Je, unaelewa kwa undani muktadha wa kitamaduni na kidini, kilingana na ukatili wa kijinsia, na siasa za familia ili kuelewa hatari ambazo wale unaowahoji wanaeza kukumbwa nazo? [Tazama #2]
  • Je, unafahamu sheria za mitaa katika eneo hilo na athari yoyote ambazo zinaweza kutokea kwa kufichua utambulisho wa wale unaowahoji na uwezo wao wa kutafuta hatua za kisheria ikiwa wataamua hivyo? (Katika baadhi ya mamlaka, mtu aliyebakwa anaweza kushtakiwa kwa hatia ya uzinzi).
  • Je,  wewe mwenyewe uko tayari kisaikolojia? Je, uko kwenye nafasi nzuri kufanya hii kazi wakati huu? [Tazama #6]

Utayari wa kawaida 

Aina nyingine ya maandalizi yanahitaji uangalifu kwa hivyo kuna mambo yanahitajika kupanga kabla ya kazi maalum. Kwa kawaida, inafaa kushiriki katika mafunzo husika lakini kama haiwezekani, kuna njia zingine kama vile kujisomea mwenyewe au ushauri mzuri kutoka kwa wenzako wenye ujuzi zinaweza kuwa muhimu sana.

Jiulize:

  • Je, unayo mpango madhubuti wa usalama wa kidijitali wa kulinda wale unaowahoji wasitambulike? [Tazama kisanduku cha rasilimali #2]
  • Je, umefanya utafiti wa mikakati wa kuhoji watu walipataa na kiwewe ambao ni wahasiriwa wa ukatili wa kingono? Kuna mambo maalum hapa ambayo unapaswa kujua. [tazama #4 na #5]
  • Je, unaelewa kikamiifu idhini ifaayo, na je, umefikiria jinsi ya kuipata? [Tazama #3]
  • Ikiwa unapiga picha au unachukua video je, umefikiria juu ya jinsi ya kuficha utambulisho na jinsi ya kuwafanya wahasiriwa kujihisi bila wasiwasi? [Tazama #8]

MAZINGATIO KWA WAHARIRI

Wakati wa mchakato wa mashauriano ya kutengeneza miongozo hii, kila mtu tuliozungumza naye wakiwemo wahariri na wanahabari walio katika nchi zilizoathiriwa na ukatili na pia wale wanaoishi nje, wote walionyesha jukumu ambalo wahariri na watayarishaji wa filamu wanayo katika kulinda wanaowahoji. Wanahabari walio uwanjani hawafanyi kali bila watu wengine kwani wanawajibika kwa wakuu wa magazeti au vituo vya utangazaji. 

Umbali kati ya walito ofisini  na wale walio unaweza kuwa tatizo kubwa. Kwa kuwa kuna masafa kati ya chumba cha habari na pahali pa matukio, kuna uwezekano wa kukosa hisia ya kuhukumu vizuri kuhusu tukio. Lakini inaweza pia kumaanisha uelewa mdogo wa muktadha na uwezekano wa kudhuru wahasiriwa. Wakati mwingine kuna shinikizo kwa waandishi wa habari katika uwanja kupata habari kwa njia yoyote. 

Vivyo hivyo, wahariri hawana habari kamili ya kile kinachotokea uwanjani. Wanahabari na watengenezaji wa filamu kawaida hufanya kazi chini ya shinikizo kubwa na wanaweza kuwa walisafiri umbali mrefu kwa hatari kubwa ya kibinafsi. Wakati mwingine wanahabari huria wanatumia pesa zao kufika katika eneo la mizozo. Katika hali hizi, wanaweza kujikuta wanatumia njia za mkato. Kwa mfano, mahojiano yanaweza kuwa ya kupindukia, kukosa kupata idhini inayofahamika kwa uzuri, kutochukua hatua za kutosha kulinda kutokujulikana kwa wahasiriwa. 

Kuwepo kwa mawasiliano bora kunaweza kusaidia kuzuia hatari kama hizi. Waandishi wa habari wanahitaji kuhisi kuwa wanaweza kuwaeleza wasiwasi kwa wahariri wao, na kwamba hawataadhibiwa kwa kuweka usalama wa mwili na wa kihemko yawahasiriwa kuliko lengo la kupata habari. 

Tutaangazia masuala haya kwa kina zaidi katika mwongozo huu. Lakini hapa kuna orodha fupi kwa wahariri wanaowapa wanahabari majukumu ya kuripoti habari zinazohusiana na ukatili wa kingono kwenye migogoro:

  • Je, umejadili sheria za msingi waandishi wa habari wanatarajiwa kufuata wakati wa kufanya kazi na waathirika wanyonge?
  • Je,  umepanga vizuri namna ya kutumia picha kwa njia ambayo inaweza kulinda utambulisho na hadhi ya mwenye kuhojiwa? Hii sio rahisi kuamua kwa wakati huu.

  • Je, hii kazi ni mwafaka kwa mwanahabari hivi sasa? Je, kuna hatari ya kazi nyingi kupita kiasi kutokana na kutoa ripoti nyingi kwa mfululizo?
  • Je, wandishi wa habari wanafahamu kama wanaweza kujadili maswala yoyote ya kimaadili na wewe?
  • Je, mwandishi ametumia muongozo kama huu?

Na mwishowe, umefikiria kutoa mafunzo yanayofaa kwa wanahabari katika kuhoji wahasiriwa wa kiwewe? Kwa bahati mbaya, hiki si kitu ambacho kwa kawaida hujumuishwa katika mafunzo ya mazingira ya uhasama. Unaweza kupata habari zaidi kuhusu ni nini shirika lako linaweza kufanya kusaidia na kulinda wanahabari wanaoshughulikia habari zinazohusiana na kiwewe kwa kushauri mwongozo huu.  

Sehemu ya #7 na #8 zinajadili masuala yanayohusika na uchapishaji na matangazo kwa undani zaidi. 

Rasimali za ziada: muhtasari

Kwanza, tuanagiza kila mtu asome rasimu ya Nambari ya Murad. Huu ni mpango ambao unaharibu kanuni bora kabisa za mazoezi kwa mtu yeyote ambaye ana mawasiliano ya moja kwa moja na wahasiriwa  wa unynyasaji wa  kwenye maeneo za migogoro -iwe ni mwandishi wa habari, wakili,  mchunguzi wa makossa ya jinai, mtunga sera, ao wakili ao wakili wa shirika lisilo la serkali. Ni zao la kushauriana kwa kina na vikundi vya wahasiriwa pamoja na kundi za wataalamu.  Kituo cha Dart kina sehemu ya wavuti yake iliyojitolea kufunika vurugu za kijinsia. Huko, unaweza pia kupata kipeperushi hiki cha Kituo kya Dart Ulaya ambacho kinatoa muhtasari mfupi.

Maelezo ya chini:

  • a

    Hizi ni miongozo ya Kituo cha Dart iliyochapishwa kwanza mnamo 2011. ; na miongozo kadhaa iliyochapishwa na umoja wa mashirika yasiyo ya kiseralikali, Global Protection Cluster, juu ya kuripoti juu ya unyanyasaji wa kijinsia katika mazingira ya mahitaji ya kibinadamu

  • b

    Johanna E. Foster na Sherizaan Minwalla, 'Sauti za Wanawake wa Yazidi: Maoni ya Mazoea ya Uandishi wa Habari katika Kuripoti juu ya dhuruma, Ukatili wa Kijinsia wa Isis,' Mkutano wa Kimataifa wa Mafunzo ya Wanawake 67 (2018): 53-64.